SIRI YA KUNENA KWA LUGHA:UTANGULIZI.

“Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo; Bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo.”

Ufalme wa Mungu umejengwa kwenye siri (mysteries), na ni utukufu wa Mungu kuficha Jambo wakati ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo. Kila kweli unayoifahamu kuhusu ufalme wa Mungu ni kati ya siri za ufalme wa Mungu ambayo Mungu ameiachilia kwa wanadamu na haswa watoto wake walioko duniani.

Inawezekana kweli unayoifahamu sasa hivi ukadhani ni ukweli inayojulikana na kila mwanadamu aliyepo duniani laki ukweli ni kwamba sio kila kweli unayoifahamu kuhusu Mungu inafahamika na kila mtu. hata wokovu ambao Mungu ameuweka wazi kabisa kwa kila nwanadamu na kutoa mwaliko kwa kila mwanadamu bado zaidi ya nusu ya wanadamu wote waishio duniani kwa sasa hawajaupokea huo wokovu, huku maamuzi ya wengi wao yakiwa yamejengwa katika kukosa ufahamu wa hiyo kweli.

Japo ni kweli kabisa kuwa ni fahari ya Mungu kuficha Jambo, kuna habari njema kwetu Sisi tunaoamini kwani Yesu mwenyewe katika Luka 8:10

“Akasema, Ninyi mmepewa kuzijua siri za ufalme wa Mungu; bali wengine kwa mifano, ili wakiona wasione, na wakisikia wasielewe.”

Ukweli huu ni ukweli wa faraja sana, kwamba sisi wa ufalme huu hatuenendi gizani bali katika nuru kwani tumekirimiwa kuzijua Siri za ufalme wa Mungu.

Yesu anasema tena katika kitabu cha Mathayo 10:27

“Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni katika nuru;na msikialo kwa siri ,lihubirini juu ya nyumba.”

Ndugu yangu kila Siri ya ufalme wa Mungu ni funguo ya kujua Siri nyingine, na pasipo kujali muda tutakaoishi duniani au kwa kiasi gani tuta “connect” na Mungu bado mafunuo ya siri zake kwetu hayatamalizika kwani Neno la Mungu lenyewe linatuambia kuwa

“Kwa maana tunafahamu kwa sehemu ;na tunafanya unabii kwa sehemu;lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabadilika.”1Kor 13:9-10

Moja ya Siri za ufalme wa Mungu ambazo Mungu ameziachilia kwa kanisa lake ni Kunena kwa Lugha. Hii si tu kwamba ni siri bali pia ni funguo ya Siri nyingine nyingi za Mungu kwani moja ya faida anazopata mtu anayenena kwa lugha ni mafunuo ya Siri za Mungu sawasawa na 1 Kor 14 :2 inayosema;

“yeye anayenena kwa lugha anaongea na Mungu na ananena mambo ya Siri katika roho yake.

Katika mfululizo huu, Mungu amenipa neema ya kufahamu kwa undani siri hii na mimi naona vyema kukushirikisha siri hii sawasawa na maneno ya Yesu katika kitabu cha Mathayo 10:27 asemapo;

“Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni katika nuru;na msikialo kwa siri, lihubirini juu ya nyumba.”

Karibu katika mfululizo wa somo letu utakaokuwa unakujia kila siku ili tujifunze lile Roho wa Mungu analotufundisha kuhusu siri hii ya kunena kwa Lugha.

Mungu akubariki sana, Tafadhali tuonane katika somo linalofuata.

Unaweza pia kumshirikisha ndugu, jamaa au rafiki kwa kubonyeza alama ya mtandao wa kijamii unaoutumia hapa chini.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *