Somo lililopita tulijifunza kuhusu maana ya Kunena kwa Lugha. leo tunaangalia sehemu nyingine ya somo letu na tunajifunza kuhusu Chimbuko la Kunena kwa Lugha.
Kunena kwa lugha ni uweza unaoambatana na muamini kujazwa Roho Mtakatifu au kubatizwa na Roho Mtakatifu au Roho Mtakatifu kuja juu yake.
Maneno hayo yote hapo juu (yaani kujazwa Roho Mtakatifu, kubatizwa na Roho Mtakatifu au Roho Mtakatifu kuja juu ya muamini) yanamaanisha kitu kimoja ambacho Yesu alikimaanisha katika Mdo 1:8 aliposema;
“Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”
Au kama yalivyonenwa na nabii Yohana Mbatizaji katika Matayo 3 : 11 akisema
” Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.”
Uzoefu huu wa kubatizwa na Roho Mtakatifu au kujazwa roho mtakatifu huja baada ya mtu kuokoka. ushahidi wa maandiko unaonyesha kubatizwa/kujazwa na Roho Mtakatifu ni uzoefu tofauti na kuokoka.
Tunaona katika kitabu cha Mdo sura ya nane(8) Filipo baada ya kuwahubiria watu wa samaria na kuipokea injili, anawaalika Mtume Petro na Yohana mwenda samaria ili kuwaombea watakatifu wale ili wabatizwe/ wajazwe na Roho Mtakatifu.
Pia katika Mdo 19:2-6 Tunaona Paulo akiwa efeso anakutana na waamini na ;
“2 akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.
3 Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana.
4 Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu.
5 Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.
6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.”
Maelezo ya Petro katika Mdo 2:14-18 pia yanathibitisha kuwa chimbuko la Kunena kwa Lugha ni Ujazo/ Ubatizo wa Roho mtakatifu.
“14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu.
15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana;
16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli,
17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.
18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri.”
Ili kuelewa ubatizo wa Roho Mtakatifu ni vizuri kufahamu uhusiano wa Roho Mtakatifu na Mwanadamu. Roho Mtakatifu anaweza kuhusiana na mwanadamu kwa namna kuu Nne.
1. Kushuhudia Ulimwengu (wanadamu ambao hawajaokoka) kwa habari ya Dhambi, Haki na Hukumu sawasawa na Yohana 16:8-11;
1. Kushuhudia Ulimwengu (wanadamu ambao hawajaokoka) kwa habari ya Dhambi, Haki na Hukumu sawasawa na Yohana 16:8-11;
“8 Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.
9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi;
10 kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena;
11 kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.”
2. Usaidizi, Ushauri, kufundisha n.k pale unaoookoka na yeye kuingia ndani yako sawaswa na Yohana 14:16-17
“16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.”
3.Kuwa katikati ya waamini.
Matayo 18:20
“Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.”
Yohana 14:17
“17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.”
4.Kuwa Juu ya Muamini. Sawa sawa na Mdo 1:8
“Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”
Mathayo 3: 16
“Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;”
Luka 4:18-19
“18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.”
Roho mtakatifu anapokuwa juu ya muamini, ndipo ubatizo wa Roho Mtakatifu unapokuwa umetokea na lengo lake kuu ni kumpatia nguvu mhusika ili aweze kuwa shahidi wa Yesu.
Ushahidi wa maandiko kama tunavyoendelea kujifunza unaonyesha kuwa katika wakati huu ndipo muamini anapopokea na lugha ya Roho Mtakatifu.
Maneno aliyoyasema Yesu katika mdo 1:8 yalitimizwa katika mdo 2 : 1- 4
” Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.
Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.
Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.
Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.”
Tunaona katika mdo 1:8 Yesu anawaahidi wanafunzi kuwa Roho Mtakatifu akiwajilia juu yao watapokea nguvu nao watakuwa mashahidi.
Sasa hebu tuangalie kilichotokea kwenye Mdo 2:1-4
- Kwanza tunaona uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi na kuijaza nyumba yote.
- Ndimi zilizogawanyikana , kama ndimi za Moto ukiowakalia kila mmoja wao.Wote wakajazwa Roho Mtakatifu.
- Wakaanza kusena kwa Lugha nyingine kama Roho alivyowajalia kutamka.
Kwa hiyo tukisoma vizuri mdo 1:8 unaona ahadi baada ya kujazwa ni nguvu na ukisoma mdo 2:4 kikichotokea baada ya kujazwa Roho Mtakatifu ni kusema kwa lugha nyingine. Hivyo basi kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya nguvu na kunena kwa lugha. na kama hivyo ndivyo basi inatupasa kujifunza siri ya kunena jwa lugha haswa kwa kuihusianisha na Nguvu za Roho Mtakatifu.
Mungu akubariki sana, Tafadhali tuonane katika somo linalofuata.
Unaweza pia kumshirikisha ndugu, jamaa au rafiki kwa kubonyeza alama ya mtandao wa kijamii unaoutumia hapa chini.